Kuunganisha Tanzania na Nishati ya kesho
Tanzania na Umoja wa Ulaya wanaimarisha ushirikiano wao ili kuongeza kasi ya kuhamia kwa nishati safi. Kama sehemu ya kampeni ya ‘Kukuza Nishati ya Kudumu Barani Afrika’, Umoja wa Ulaya inaongoza jitihada za kuzidisha mara tatu uwezo wa uzalishaji wa Nishati ya kudumu barani Afrika kufikia mwaka 2030. Kwa Tanzania hii inajumuisha uwekezaji katika mabwawa ya kuzalisha umeme uunganishwaji na usafirishaji wa umeme ili kutoa nishati safi, nafuu na ya kudumu. Jitihada hizi zitaleta athari chanya katika maisha ya watu leo na kesho.
Kutana na Ahmed
Mimi ni Ahmed, na ninaendesha biashara ya baa yenye mandhari ya kipekee iliyoko Bahari Beach, Dar es Salaam. Wageni huja kufurahia muziki, kucheza mchezo wa biliadi au kupumzika kando ya bahari, Baa yangu ni kitovu cha burudani na uchangamfu.
Leo nina furaha kuona kwamba Nishati ya kudumu inafanya umeme uwe wa uhakika zaidi, kwa sababu kama vile tu burudani nzuri ya kujivinjari usiku, Nishati inatakiwa kuwa ya kuaminika kila wakati.
Kwa kuwa nina Nishati safi, ninaweza kuhakikisha vinywaji ni baridi, taa zinawaka na kudumisha uchangamfu wa ufukweni kila usiku. Iwapo baa yangu itatumia Nishati vizuri zaidi, sitakuwa ninahudumia tu jamii yangu, nitakuwa ninasaidia kujenga maisha bora ya baadaye, jioni baada ya nyingine.
Kutana na Fatuma
Naitwa Fatuma, nafanya kazi kwenye duka la nguo za wanaume lililoko Kariakoo, Dar es Salaam. Baada ya kusimama kwa saa nyingi, mimi huenda katika uwanja wa kandanda kufanya mazoezi na kucheza na timu yangu.
Nashukuru kwa Nishati ya kudumu inafanya vifaa vya michezo viwe vya kutegemewa zaidi, ina maana tunaweza kuendelea kufanya mazoezi chini ya taa.
Kwa kuwa na mwanga mzuri na uwezo wa kupata Nishati, ninaweza kuwa katika hali nzuri kila wakati na kuendelea kufuata ndoto yangu. Kadri uwezo wa kupata Nishati unavyozidi kuboreka, nitaweza kuendelea kucheza mchezo wa kupendeza, kwa ajili ya vizazi vijavyo vya Tanzania.
PARTNERS
Nora Daniel
Nora Daniel ni mtayarishi mtanzania wa maudhui ya usafiri na mitindo ya maisha anayetumia teknolojia dijitali kudhihirisha masimulizi. Kupitia nguvu ya majukwaa ya mitandao ya kijamii, hutayarisha maudhui ya ubora wa juu yanayovutia hadhira yake kugundua, kujihusisha na kuishi kwa ujasiri zaidi kupitia mitazamo yake. Huchanganya ubunifu na teknolojia ili kutayarisha maudhui ambayo ni halisi na ya kuleta athari. Kazi zake zinaonyesha jinsi watayarishi waafrika wanavyoweza kutumia zana dijitali kukuza chapa binafsi, kufikia hadhira za kimataifa na kubuni masimulizi kutokana na mitazamo yao binafsi.
Frida Amani

Frida Amani ni mwimbaji jasiri mtanzania, mtu mashuhuri katika vyombo vya habari na mtetezi wa mazingira anayetumia sauti na usanii wake kuleta mabadiliko ya kijamii katika Afrika Mashariki. Kwa kuchanganya muziki na shughuli za utetezi, huelekeza usimuliaji wenye nguvu katika kuangazia masuala ya uwezeshaji wa wanawake, utunzaji wa mazingira na haki katika jamii. Kupitia kazi yake, Frida hupinga desturi za kawaida, huchochea kuchukua hatua na huwezesha jamii zilizotengwa kupaza sauti zao. Uwepo wake wa kijasiri katika nyanja za ubunifu na kiraia unamfanya awe nguvu kuu ya kuleta mabadiliko katika mazingira ya utamaduni na utetezi katika kanda.
Scaling up Renewables in Africa campaign
Bara la Afrika lina uwezo wa kuwa bara lililoendelea zaidi duniani. Lakini licha ya uwezo huu, mamilioni ya watu barani bado hawana uwezo wa kupata umeme. Kadri mabadiliko ya tabianchi na idadi ya watu barani Afrika inavyozidi kuongezeka, kampeni ya ‘Kukuza Nishati ya Kudumu Barani Afrika’ inalenga kufungua uwezo huo. Juhudi hizi zinalenga kuleta Nishati nafuu, ya kudumu na ya kutegemewa kwa watu wa Afrika, huku ikiunda nafasi za kazi na kuendeleza ukuaji wa kudumu.
MIPANGO YA NISHATI NCHINI TANZANIA
Mtambo wa uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya maji kwa nishati safi Tanzania
Kwa msaada wa Umoja wa Ulaya chini ya Global Gateway, mtambo wa uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya maji wa Kakono utazalisha 87 MW za umeme jadidifu—unaowafikia takribani watu milioni 3. Mradi unasaidia katika ukuaji wa uchumi, ajira na malengo ya tabia nchi kwa kupunguza utegemezi wa mafuta na kutoa nishati nafuu kwa kaya na viwanda.
Kuongeza uwezo wa ujumuishaji wa nishati kwa uunganishwaji wa nchi za Zambia–Tanzania–Kenya
Mradi huu wa Global Gateway unaunganisha gridi za nishati za nchi tatu, na kuwezesha ubadilishanaji wa nishati endelevu na nafuu. Unaongeza uwezo wa ulinzi wa nishati wa kanda na kuwezesha ufikiwaji mkubwa zaidi wa nishati safi kwa mamilioni ya watu Afrika Mashariki.
Kujenga miundombinu imara ya nishati Ifakara na Kilombero
Kwa msaada wa Umoja wa Ulaya chini ya Global Gateway, kituo kidogo cha kusambaza pamoja na njia mpya za usambazaji zenye urefu wa km 70 vitaboresha usambazaji wa umeme kwa zaidi ya watu 60,000 katika wilaya ya Kilombero nchini Tanzania. Mradi unawezesha uhakika, kusaidia biashara na kuchangia katika maendeleo ya mkoa.
Unaziunganisha kwenye umeme jamii za vijijini nchini Tanzania
Mpango huu wa kuunganisha umeme vijijini unaowezeshwa na Umoja wa Ulaya unaongeza mawanda ya gridi ya taifa na kuanzisha gridi ndogo katika maeneo yasiyofikiwa ukisaidia zaidi ya watu 110,000 kufikia nishati safi, ya uhakika. Unawezesha jamii kukuza uchumi, na kuboresha ufikiwaji wa huduma za muhimu.
Kupanua ufikiaji wa umeme kwa jamii za kipato cha chini za kaskazini magharibi mwa Tanzania
Mradi wa umeme wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania unaunganisha kaya zenye kipato cha chini katika ukanda wa Geita-Nyakanazi ukiwezesha ufikiaji wa nishati kwa maelfu ya watu. Msaada wa Umoja wa Ulaya unasaidia kupunguza gharama ya uunganishaji kwa familia, na kuwezesha ujumuishwaji na fursa za kiuchumi.
Kuboresha sekta ya nishati Tanzania kwa ajili ya ukuaji endelevu
Mradi huu unaowezeshwa na Umoja wa Ulaya unasaidia kuboresha mpango na sheria za matumizi ya kitaifa ya nishati. Kwa kuhuisha mfumo na kujenga uwezo, mpango unawezesha uhakika wa nishati na ufanisi - ukifaidisha kaya, biashara, na uchumi kwa ujumla.
Unawawezesha Watanzania kupata njia safi za nishati ya kupikia kwa ajili ya afya njema na kuhifadhi mazingira
Mradi huu unaowezeshwa na Umoja wa Ulaya unaunga mkono njia endelevu za nishati ya kupikia hivyo kuboresha maisha ya zaidi ya watu milioni 5. Unapunguza ukataji miti na uchafuzi wa ndani wa hewa, kuwawezesha wanawake, na kuchangia matokeo chanya ya afya njema na uhifadhi wa mazingira.
Kuongeza njia endelevu za matumizi ya nishati nchini Tanzania
Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Nishati Fanisi wa Tanzania unaoungwa mkono na Umoja wa Ulaya umewapa mafunzo zaidi ya mameneja 130 na kutambulisha viwango vya utendaji kwa ajili ya majengo na vifaa vya umeme. Maboresho haya yanasaidia kupunguza upoteaji wa nishati, kupunguza uchafuzi wa mazingira na kupunguza gharama za umeme katika kaya na viwandani.