Taarifa ya Pamoja kabla ya uchaguzi mkuu wa Kenya wa 9 Agosti 2022

Sisi, wakuu wa misheni ya uangalizi wa uchaguzi, tumekuwa tukifuatilia maandalizi ya uchaguzi kwa washikadau wote wa uchaguzi mkuu wa Kenya wa Agosti 9, ikijumuisha kampeni za vyama vya kisiasa, miungano ya vyama na wawaniaji. Tunawahimiza viongozi wa vyama vyote vya kisiasa na wafuasi wao, pamoja na asasi za kiraia, na washikadau wengine wote kuhakikisha uwepo wa mazingira ya utulivu na amani kwa muda uliosalia wa mchakato wa uchaguzi.

Tunawaomba pia watu wote wenye mamlaka maalum wakati wa uchaguzi wa Agosti 9 kuwajibika kwa uwazi; Pamoja na kufuata mfumo wa sheria wa Kenya, kwa ajili ya uchaguzi wa kidemokrasia. Mwisho, tunawahimiza washikadau na wananchi wote kufuatilia malalamiko ambayo yanaweza kutokea kwa njia ya amani na kisheria.

Tunapoendelea kuangalia maandalizi ya uchaguzi kote nchini, tunaungana kwa pamoja na Wakenya kwa matamanio yao ya uchaguzi wa amani na wa kuaminika.

1. Ujumbe wa pamoja wa waangalizi wa uchaguzi wa AU na COMESA–Mheshimiwa Dkt. Ernest Bai Koroma, rais wa zamani wa Sierra Leone.

2. Ujumbe wa uangalizi wa uchaguzi wa Kituo cha Carter – Ben Graham Jones, Kiongozi wa kundi.

3. Kundi la uangalizi wa uchaguzi  la Jumuia ya Madola – Mheshimiwa Bruce Golding, Waziri mkuu wa zamani wa Jamaica.

4. Ujumbe wa Uangalizi wa Uchaguzi wa EISA– Mheshimiwa Goodluck Ebele Jonathan, rais wa zamani wa Nigeria.

5. Ujumbe wa Uangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya- Mheshimiwa Ivan Štefanec, Mbunge wa Bunge la Ulaya.

6. Ujumbe wa Uangalizi wa Uchaguzi wa IGAD- Mheshimiwa Dkt. Mulatu Teshome, rais wa zamani wa Ethiopia.

7. Ujumbe wa uangalizi wa uchaguzi wa IRI/NDI- Mheshimiwa Joaquim Chissano,rais wa zamani wa Msumbiji.