Sorry, you need to enable JavaScript to visit this website.

Mwanzo wa Usalama wa Chakula: Hadithi ya Shamba Moja la Ukraine

Hryhorii Tkachenko aliporejea kwenye shamba lake, jambo la kwanza aliloona ni kazi ya maisha yake ikiwa imesambaratika.

Ng'ombe waliokufa walikuwa wametapakaa shambani. Mashine zilikuwa zimeharibiwa. Mabanda yalikuwa yamebomoka. Kituo cha kisasa cha kukamulia, ambacho hapo awali kilikuwa kitovu cha shughuli za kila siku za shamba, kilikuwa kimeharibika kabisa. Mashamba yaliyopaswa kutayarishwa kwa ajili ya kupanda ngano, mahindi na alizeti hayakuwa salama — mabomu ya ardhini na makombora ambayo hayakuwa yamelipuka yalikuwa yametapakaa kote, na kufanya isiwezekane kuingia humo kwa usalama.

Soma taarifa kamili

 

Jinsi Urusi inavyofanya kampeni katika maeneo yaliyovamiwa ili kuhamasisha watu kujiunga na jeshi lake

Katika maeneo yaliyovamiwa kwa muda ya Mikoa ya Luhansk na Donetsk, Urusi inatekeleza uhamasishaji wa kulazimishwa huku ikiendesha kampeni kikamilifu kuwashawishi wakazi wa eneo hilo kujiunga na vikosi vyake vya kijeshi. Juhudi hizi zinalenga kuongeza idadi ya wanajeshi katika jeshi la Urusi kwa ajili ya vita dhidi ya Ukraine. Ili kufanikisha hilo, mamlaka bandia hutumia mbinu mbalimbali za ushawishi na njia tofauti za mawasiliano.

Endelea kusoma ili kupata muhtasari wa jinsi wakazi wanavyohimizwa kujiunga na jeshi, pamoja na mbinu za uajiri na zana za propaganda zinazotumika kwa sasa.

Mkataba au jela: Jinsi Urusi inavyowashawishi wakazi wa eneo la Zaporizhzhia lililovamiwa kujiunga na jeshi lake

Jinsi wavamizi wanavyotekeleza uajiri na uhamasishaji wa lazima

Andriy mwenye umri wa miaka 17 (jina limebadilishwa kwa sababu za kiusalama), kutoka sehemu ya eneo la Zaporizhzhia iliyovamiwa, alisimamishwa kwa ajili ya ukaguzi wa simu, hakutarajia kamwe kwamba jambo hilo lingempeleka kwenye jeshi la Urusi.

Warusi waliingia katika eneo la Zaporizhzhia tarehe 24 Februari 2022, siku ya kwanza ya uvamizi kamili wa Ukraine. Kufikia siku iliyofuata, walikuwa wamechukua rasmi udhibiti wa Melitopol, jiji kubwa zaidi katika eneo hilo baada ya Zaporizhzhia.

Soma taarifa kamili

Jinsi Urusi inavyowafukuza Waukraine kutoka kwenye makazi yao

Uadilifu wa eneo

"Hutaweza tena kuutambua mji huu. Hauhisi tena kama ni wetu—unahisi kama ni wa kigeni. Watu ni tofauti. Unasikia lafudhi ya Moscow au Kirusi kinachozungumzwa kwa shida. Sitambui tena Mariupol," anasema Olha.

Soma taarifa kamili

Jinsi vita vilivyoharibu michezo mashariki mwa Ukraine

Uadilifu wa eneo

Hadi hivi karibuni, mashariki mwa Ukraine ilikuwa mojawapo ya vituo muhimu vya michezo nchini humo. Timu ya Shakhtar Donetsk ilikuwa ikishiriki mara kwa mara katika Ligi ya Mabingwa, Uwanja wa Donbas Arena uliandaa mechi za Euro 2012, na klabu za soka, mpira wa magongo ya barafu na mpira wa kikapu za eneo hilo zilishindana katika ngazi ya juu kabisa. Maelfu ya watoto walifanya mazoezi katika akademia za michezo, wakiota siku moja kucheza katika viwanja vikubwa.

Soma taarifa kamili

 

 

 

 

 

“Si Chako – Ndiyo Maana una Hasira”

Uadilifu wa eneo

Katika mchoro mmoja kutoka Shajara za Mavka — ushuhuda wa wanawake wasiojulikana wenye taswira kuhusu maisha chini ya uvamizi wa Urusi, unaochapishwa kupitia mtandao wa siri wa “Angry Mavka” — mwanamke aliyefunika uso anainua kipande cha karatasi kilichoandikwa kwa Kirusi: Не твоя, вот и бесишься: si chako, ndiyo maana una hasira. 

Soma makala kamili

 

Unyanyasaji wa pasi ya kusafiria

Uadilifu wa eneo

Mykola (si jina lake halisi) alipofika hospitalini katika eneo la Ukraine lililotekwa na Urusi akiwa na ngiri kali, alitarajia madaktari waratibu upasuaji. Badala yake, aliambiwa kuwa hangeweza kutibiwa hadi awe raia wa Urusi.

“Kama ungependa kuishi, pata pasipoti,” daktari alimwambia.

Soma makala kamili

 

 

Mapambano yasiyo na matumaini ya kudai mali zilizotaifishwa katika maeneo ya Ukraine yaliyovamiwa

Uadilifu wa eneo

Olena (jina limebadilishwa) alipokimbia Melitopol kusini mwa Ukraine mwanzoni mwa Machi 2022, alifunga nguo za watoto wake wawili, akafunga mlango wa mbele wa nyumba yao ya ghorofa mbili, na kumpa jirani aliyemwamini funguo ya ziada. 

Soma makala kamili

 

Kula Mwisho.

Shughuli ambazo Watu Hufanya Kupata Chakula Katika Maeneo Yaliyovamiwa

Katika Oleshky, mji katika mkoa wa Kherson ambao umekuwa chini ya uvamizi tangu siku ya kwanza ya uvamizi kamili, majira ya baridi ya 2025–2026 yalijibu swali ambalo sehemu kubwa ya Ulaya haikukabiliana nalo kwa vizazi kadhaa: nini hutokea pale ambapo bidhaa na mahitaji ya msingi yanapoacha kuwasili? Mji huo umekuwa chini ya uvamizi tangu Desemba 2025. 

Soma taarifa kamili

 

Chakula Chini ya Udhibiti.

Jinsi utekwaji wa Mariupol ulivyofanya eneo la kusini mwa Donetsk kutegemea Urusi

Baada ya kutekwa kwa Mariupol, Urusi haikubadili tu mamlaka, hati na bendera za jiji hilo. Ilivunja pia mojawapo ya mifumo ya msingi ambayo maisha ya kila siku ya watu hutegemea: upatikanaji wa chakula.

Ugavi wa chakula ya Ukraine ilikatizwa. Mitandao ya rejareja iliyokuwapo kabla ya vita ilitoweka au ilianza tena kufanya kazi kwa majina tofauti. Rafu za maduka zilijazwa bidhaa kutoka Urusi na Belarus.

Soma taarifa kamili

 

Mashamba Yaliyotekwa, Nafaka Iliyoibiwa

Jinsi Urusi Inavyotumia Kilimo kwa Manufaa Yake Kusini mwa Ukraine

Katika majira ya kiangazi ya mwaka wa 2022, katika kijiji cha Mangush, kilichoko kilomita 25 kutoka Mariupol, wakazi wa eneo hilo walikuwa wakiuza chupa za mvinyo kutoka Vyna Pryazovia, kiwanda cha mvinyo cha Ukraine kilichokuwa katika eneo hilo. Mvinyo huo, uliotengenezwa kutokana na zabibu za mavuno ya mwaka wa 2020, ulikuwa ukiuzwa kwa bei ya chini sana—licha ya kuwa ulikuwa umeshinda medali tano za dhahabu katika maonesho yaliyofanyika Verona katika katika mwaka wa 2021. 

Soma taarifa kamili.

Uaminifu Ndiyo Rasilimali Kuu ya Wakati wa Vita

Kwenye skrini yangu kuna umbo ambalo si rahisi kutambua: kofia iliyovutwa chini, uso ukiwa umefichwa, na sauti yake imepitishwa kwenye kichujio cha sauti bandia hadi kuwa katika hali ile ya sauti bapa ambayo wengi wetu tunaifahamu kwenye video fupi. 

Soma taarifa kamili

Wakati pengo kati ya uhalisia na televisheni linakuwa kubwa kupita kiasi, propaganda hupoteza nguvu yake

Oksana, mwanamke kutoka Mariupol, ni muuguzi. Alizaliwa nchini Ukraine na ameishi Mariupol tangu kuzaliwa, ingawa familia yake asili inatoka eneo la Samara nchini Urusi. Kwa hivyo, ingawa Oksana alikuwa na pasipoti ya Ukraine, alijiona kuwa Mrusi. 

Soma taarifa kamili

“Chumvi haina ladha, sukari si tamu.”

Jinsi uvamizi ulivyobadilisha bidhaa madukani na kilichobaki kwenye rafu baada ya 2014

Uvamizi wa Urusi katika maeneo ya mashariki mwa Ukraine ulianza katika mwaka wa 2014. Katika kipindi hiki, Warusi wamejaribu kuondoa kila kitu cha Kiukraine katika nyanja zote za maisha, na sekta ya chakula haijaachwa nyuma. Sasa, badala ya bidhaa za Kiukraine, bidhaa za Urusi au zilizoagizwa kutoka nchi “zinazoichukulia Urusi kwa urafiki” zinapatikana kwenye vibanda vya masoko na rafu za maduka makubwa. Watu hulalamika kuhusu uduni wake na kutamani bidhaa zao wanazozipenda kutoka kwa wazalishaji wa Kiukraine, lakini hawana chaguo kubwa. 

Soma zaidi ili kufahamu jinsi maisha yalivyobadilika katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa muda wa Urusi (TOT), kupitia simulizi za watu waliokulia huko.

 

Vita na Biashara

Jinsi Uvamizi wa Donbas Ulivyoathiri Uhusiano wa Kiuchumi wa Ukraine na Kenya na Malaysia

Kwa zaidi ya miaka 30, Ukraine imekuwa ikiendeleza uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na Jamhuri ya Kenya na Malaysia. Bidhaa za kilimo na metallojia zilikuwa na nafasi muhimu katika mauzo ya nje ya Ukraine kwenda katika nchi hizi. Biashara na sekta ya kilimo katika mikoa ya Donetsk na Luhansk zilitoa mchango mkubwa katika kujenga uwezo huu wa kuuza bidhaa nje ya nchi. 

Soma taarifa kamili

 

 

Filamu na televisheni za Urusi zinachukua nafasi ya vyombo vya habari vya Ukraine: jinsi adui anavyobadili utambulisho chini ya uvamizi

Wakati kumbi za sinema zinapofungwa katika maeneo yaliyovamiwa, mara nyingi huonekana kama matokeo mengine ya vita — majengo kuharibiwa, kukatika kwa umeme, au ukosefu wa watazamaji. Hata hivyo, kumbi ambazo bado zinafanya kazi zimebadilishwa: hazionyeshi tena filamu za Ukraine au za kimataifa, bali zinatumika kama majukwaa ya propaganda na upotoshaji wa fikra.

Soma taarifa kamili

Upungufu wa Taarifa

Habari and uhuru wa kusema

Kwa familia nyingi zinazoishi katika maeneo yaliyotekwa na Urusi, elimu si suala la kujifunza pekee tena. Imekuwa mojawapo ya njia zao za mwisho zilizosalia za kuendelea kuunganishwa na Ukraine.

Kwa usiri mkubwa na kwa kutumia mtandao binafsi wa faragha, watoto wa Ukraine huingia kwenye madarasa ya mtandaoni. Wengine husubiri hadi usiku wa manane, wakati vizuizi vya intaneti vinapolegezwa, wakitumai kutuma kazi zao walizokamilisha kwa walimu walioko katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali ya Ukraine. 

Soma taarifa kamili

Read more articles